Sekta ya Utalii nchini imeandika Historia mpya baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt Hamis Kigwangala kuweka rekodi ya kuwa Waziri wa kwanza wa Wizara ya Maliasili na Utalii kufika katika Kilele kirefu barani Afrika,Kilele cha Uhuru ,umbali wa mita 5895 kutoka usawa wa bahari.