Kelvin John afunguka baada ya kunyakua tuzo

Kelvin John ambaye ndiyo mfungaji Bora wa michuano ya CECAFA na mchezaji Bora amesema kuwa tuzo hizo ameipata kutokana na ushirikiano wa wachezaji kiujumla.

John amefunga jumla ya mabao saba kwenye michezo mitano ambayo wamecheza na walitwaa kombe la CECAFA kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kenya kwenye michuan hiyo iliyofanyika nchini Uganda.

"Ni furaha kuona malengo ya timu yamekamilika na tunaamini ni kutokana na maombi pamoja na ushirikiano ndivyo vinavyotupa mafanikio," amesema.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia