Na John Walter-Babati
Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijjni, Vrajil Jituson ameendelea kuwaboreshea Wananchi wake miundo mbinu pamoja na huduma za kijamii ili waendelee kushiriki kikamilifu katika shughuli za kuwaletea maendeleo wao na taifa kwa ujumla.
Miundo mbinu iliyoboreshwa na Mbunge huyo ni pamoja na shule za msingi,Sekondari,Hospitali pamoja na Zahanati ikiwa ni mpango wake wa kuhakikisha wakina mama,watoto,vijana na wazee wanapata huduma bora za afya huku wanafunzi wakisoma kwenye mazingira rafiki.
Jituson ametoa Mifuko elfu moja na mia mbili (1,200) za Saruji yenye thamani ya shilingi Milioni kumi na sita na laki mbili (16,200,000) ikiwa ni awamu ya pili kufanya hivyo.
Ikumbukwe kwamba awamu ya kwanza mapema mwezi January mwaka 2019,Mheshimiwa Jituson tayari alishatoa zaidi ya Sh.milioni 60 kutoka Mfuko wa Jimbo kwenye kata 25 ili kuweza kuchangia kasi katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo zikiwemo shule za msingi.
Baadhi ya Viongozi wa serikali na wanasiasa katika Halmashauri ya wilaya ya Babati wameipongeza hatua ya Mbunge huyo wakisema ni viongozi wachache wenye moyo huo wa kujitolea.
Mtendaji wa kijiji cha Hoshan Dickson John akizungumza kwa niaba ya wananchi amesema amepokea mifuko hamsini ya Saruji ambayo wanategemea itakwenda kukamilisha Zahanati hiyo kwa hatua ya msingi na Ukuta hivyo wadau wengine wajitokeze ili kukamilisha Zahanati hiyo na ianze kutumika.
Kwa upande wa mwakilishi wa mtendaji wa wakijiji cha Boay Emmanuel Peter amesema wamepokea mifuko mia mbili ambayo wanakwenda kukamilisha ujenzi wa madarasa katika shule ya Sekondari Boay ,Nyumba za walimu na matundu ya Vyoo.
Naye Hassan Mohamed Bakari Afisa Mtendaji wa kijiji cha Hoshan, amesema alichokifanya Mbunge huyo ni jambo la Kizalendo na la kuigwa na viongozi wengine katika jamii ili kuwa na taifa lenye maendeleo.
Mbunge Jitu analiongoza jimbo hilo linalopatikana katika mkoa wa Manyara lenye kata 25 na Tarafa nne,yaani Ghorowa,Bashnet,Babati pamoja na Mbugwe.

