Rais Magufuli ammwagia sifa Mizengo Pinda 'ndio maana nimemchagua'


Rais wa Tanzania, John Magufuli amesema Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda ana msaidia sana kati ya viongozi wastaafu wanaomsaidia kuongoza nchi.

“Leo ilitakiwa awepo hapa Mzee Pinda ananisaidia sana katika kazi, yule baba ana moyo wa kipekee,” Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo mkoani Katavi wakati wa uzinduzi wa barabara ya Kanazi-Kizi-Kibaoni.

“Ni mtu mwema sana  na ndio maana nimemchagua kuwa  mjumbe wa  kamati kuu. Ananisaidia kuongoza nchi, chama katika mambo mbalimbali kwa sababu ni mtu mmoja mstaarabu sana,”

Ameongeza, “Na ndio maana nimemtuma China akaniwakilishe katika maadhimisho ya miaka 20 ya kifo cha mwalimu Julius Nyerere. Niliona  sina mwingine wa kumtuma atakayeniwakilisha vizuri nikasema Mizengo Pinda ndio aende, ni baba mwenye moyo wa tofauti.”