Na. Baraka Messa, Songwe
Marais wawili wa Tanzania John Magufuli na Edgar Lungu wa Zambia kwa pamoja wamekubaliana kuboresha mpaka wa nchi hizo mbili ili kuimalisha biashara na kukuza uchumi wa nchi hizo.
Wameongea hayo wakati wa kufungua kituo cha Huduma kwa pamoja mpakani Tunduma Tanzania na Nakonde Zambia.
Rais Magufuli alisema miradi ambayo nchi hizo ziliianzisha waasis Julia's Nyerere na Keneth Kaunda kwa upande wa Zambia kama vile bomba la Mafuta TAZAMA na TAZARA yote haiendi vizur na kukwamisha uchumi.
Dkt Magufuli alisema Zambia ndio nchi inayoongoza kuchukua mizigo kupitia bandari ya DaresSlaam kwa asilimia 38, hivyo alisema ni vema kushirikiana nao kutokana na kushirikiana vizur kiuchumi.
Alisema wameamua kuungana kwa pamoja ili kukuza biashara ndani ya jumuiya ya nchi za kusini SADC kwa kupitia mipaka inayotengsnisha.
Dkt Magufuli alisema wananchi wore ambao wamejenga kwenye mipaka kuhama Mara moja kupisha marekebisho hayo yatakayo pelekea wafanyabiashara na wananchi kuwa salama.
"Kuna wananchi wamejenga katikati ya mpaka mlango mmoja upo Tanzania na mwingine upo Zambia , hii hupelekea kufanyika biashara haram, kuleta migogoro mibaya na na ulinzi kuwa mgumu kwa serikali hizi mbili''
Alisema lengo la kujenga kituo hicho kilicho gharimu shilingi bilioni 14 ni kuwaboreshea wananchi mazingira ya kufanyia biashara na usafirishaji wa mizigo yao.
" viongoz mnaohusika kwenye hiki kituo tulicho zindua waacheni wafanye biashara na wasafirishaji waache wafanye biashara kwa utulivu na usalama ili kumalisha undugu wetu pia , lakini pia wananchi wa Tunduma hakikisheni mnafanya biashara halali ambazo zitawaletea kipato kikubwa"
alisema Rais Magufuli
Kwa upande wake Rais wa Zambia Edgar Lungu alisema dhamira ya nchi hizi mbili ni kukuza uchumi na uhusiano ambao uliasisiwa toka enzi za Uhuru kwa nchi hizo.
Alisema 2010 nchi hizi mbili ziliianzisha mkataba wa pamoja ambao ambao umeongeza na kuimalisha uhusiano wa nchi hizi mbili.
Rais Rungu alisema kuimalika kwa kituo cha pamoja kitasaidia kupitisha malori zaidi ya 600 kwa siku moja na kuongeza ushindani wa kibiashara utakaopelekea uchumi kukua kwa nchi hizo mbili.
"Serikali zetu pia zinawathamini na kuwatambua wafanye biashara wadogo, tunawasaidia mikataba yetu inawatambua ili kuwasaidia waweze kufanya biashara bila kusumbuliwa
Aidha Lungu aliwataka wananchi wake waliojenga kwenye alama za mipaka kushirikiana na viongozi wao ili wafanye utaratibu wa kuhama kabla serikali haijatumia nguvu
