Wadau wa uchaguzi watakiwa kutokwamisha zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura


Na. Rahel Nyabali Tabora

Wakati zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya kwanza likiwambioni kuanza mkoani  Tabora tume ya taifa ya uchaguzi NEC imewataka wadau wa uchaguzi mkoani humo ikiwemo wanasiasa kutokwamisha zoezi hilo kutokana na kupotosha maelekezo pindi wanapo wafikia wananchi.


Akizungumuza Kamishina wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Asina Omari katika katikamkutano na wadau wa uchaguzi wa mkoani Tabora amesema tume inategemea kupata ushirikiano katika kufanikisha zoezi hilo na sivinginevyo.

Baadhi ya wadau walioshiriki  akiwemo  Rahema  kabata amesema Elimu hiyo waliyo pata itaweza   kuwasaidia wadai pamoja na wananchi wanao wazunguka ili kuweza kufanikishwa kwa zoezi hilo.

Aidha zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura mkoani Tabora litafanyika kwa mudawa siku saba likitarajiwa kuanza october 14 ya mwaka huu .

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia