Watu 20 wauawa kwa shambulio mgodini Burkina Faso

Takribani watu 20 wamekufa, baada ya shambulio la siku ya Ijumaa lililolenga eneo la mgodi kaskazini mwa Burkina Faso.

Kwa mujibu wa maafisa wa usalama, watu wenye silaha, walivamia mgodi huo na kuwaua watu, wengi wao wakiwa ni wachimbaji madini. Idadi kamili ya waliojeruhiwa kwenye tukio hilo hadi sasa haijafahamika. Kundi la wanajihadi linalaumiwa kufanya shambulio hilo.

Burkina Faso, imekuwa ikilengwa katika mashambulizi ya kigaidi, mengi yakihusishwa na makundi yenye mfungamano na Al Qaeda, na kundi linalojiita Dola la Kiislamu.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, zaidi ya watu 585 wameuawa kutokana na mashambulizi nchini humo, tangu mwanzoni mwa mwaka 2015.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia