Bunge la Umoja wa Ulaya lazitaka nchi wanachama kuwachukua watoto wa magaidi

Bunge la Ulaya limepitisha kuwa sheria muswada uliokuwepo uliozitaka nchi wanachama wa umoja wa Ulaya kuwachukua watoto wa wapiganaji wa makundi ya kigaidi ambao ni raia wa kigeni.

Baraza kuu la bunge la Ulaya lilikutana Strazburg na kupigia kura miswada iliyokuwepo kama vile ”Haki za watoto, Unyanyasaji, ubakaji na ndoa za lazima”. Wabunge 58 walipiga ura za hapana na 495 walipiga kura za ndio.

Katika uamuzi huo ambao unapinga kila aina ya unyanyasaji dhidi ya watoto, ulitolewa wito kwa nchi za Umoja wa Ulaya kutafuta mbinu mpya za kupambana na changamoto za kila aina ya unyanyasaji dhidi ya watoto, iwe katika maisha halisia au mitandaoni.

Katika maamuzi yanayohusu watoto wa wapiganaji wa makundi ya kigaidi raia wa kigeni huko kaskazini mashariki mwa Syria,

"Tunatoa wito kwa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya kuwachukua watoto wa wapiganaji wa makundi ya kigaidi ambao ni raia wan chi zao, kwani watoto hao wanaingia katika kundi la familia maalum”, ulisema uamuzi uliofikiwa.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia