Klabu ya Chelsea imefanikiwa kusogea hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kuipiga Crystal Palace 2-0 kwenye mchezo uliochezwa Stamford Bridge.
Magoli ya Chelsea yaliwekwa kambani na Tammy Abraham dakika ya 52 na jingine likifungwa na Christian Pulisic dakika ya 79.