China imetishia kulipiza kisasi hatua ya Rais wa Marekani ya kusaini sheria mpya inayounga mkono wandamanaji wa kupigania demokrasia mjini Hong Kong, wakati nchi hizo mbili zinazoongoza kiuchumi duniani zikielekea kupata muafaka katika mzozo wa kibiashara baina yao.
Wanaharakati hao wa Hong Kong wameikaribisha hatua ya Marekani, kwa kufanya matembezi ya kutoa shukrani kwa Rais Trump na wabunge mjini Washington.
Trump alikabiliwa na shinikizo kutoka kwa wabunge wa mabaraza mawili ya bunge, ambayo kwa mshikamano nadra wa vyama viwili, kwa kauli moja waliipitisha sheria hiyo.
Baada ya kuiidhinisha sheria hiyo Trump ametoa tangazo akisema anamheshimu rais wa China Xi Jinping, na kwamba anatarajia mzozo kati ya Beijing na Hong Kong utatatuliwa kwa njia za amani.
China iliyokasirishwa na sheria hiyo imemtaka maelezo balozi wa Marekani, na imeonya juu ya hatua kali ambazo hazikubainishwa, ikiwa Marekani itaitekeleza sheria hiyo.