Kituo cha afya Nyasubi kujengwa kwa milioni 409



Na Paschal Malulu-Kahama.

Kituo cha afya cha Kata ya Nyasubi katika Halmashauri ya mji wa Kahama Mkoani Shinyanga kinatarajiwa kutumia milioni 409 hadi kukamilika kujengwa na kuanza kutumika.

Akizungumza na Mwandishi wa Muungwana Blog mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Kahama Abel Shija amesema kituo hicho kilitakiwa kutumia milioni 260 zilizotengwa na kwenye bajeti ya halmashauri.

Amesema katika kituo hicho majengo mawili yameongezwa ambayo tayari msingi umechimbwa na ujenzi unaendelea hivyo halmashauri imeongeza milioni zaidi ya 130 za kukamilisha ujenzi wa jengo la upasuaji, jengo la mama na mtoto, vyoo na shimo la kuchomea taka.

“ujue katika kituo chetu hiki cha afya hiki ni kipya kabisa ambacho ndio kinakuja kuwa msaada kwa wananchi kupata huduma kwahiyo milioni 260 hazikutosha zikaongezwa zingine zaidi ya milioni 130 kwahiyo sio tu kusimamisha majengo yake hiyo hela milioni 409 inajumlisha hadi vifaa tiba”.

“kama unakumbuka hapo tu hospitali ya wilaya fisi walikuwa wanaingia mpaka sasa hivi hadi mbwa kwahiyo pia tutajenga na uzio lakini tunatazamia kuangalia kiasi cha fedha ambacho kitabaki ili kukitumia kujenga uzio kwa usalama wa wagonjwa”alisema Shija.

Shija amesema fedha hiyo milioni 409 haitatumika kwenye ujenzi tu isipokuwa itatumika pia kununulia vifaa tiba hivyo kwa jinsi ujenzi unavyoendelea kufikia mwakani kituo hicho kitakuwa kimekamilika na kuanza kutumika.

Aidha Shija ameongeza kuwa katika halmashauri ya mji katika bajeti yake vituo vya afya vinaendelea kujengwa ili kuhakikisha huduma za afya zinakuwa karibu na mwanachi.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia