Mfugaji nyoka akutwa amekufa huku nyoka wakiwa wamemzunguka kwenye shingo

Mwanamke mmoja amekutwa amekufa katika jimbo la Indiana nchini Marekani ahuku nyoka mwenye sumu akiwa amemzunguka katika shingo.

Laura Hurst ambaye alikuwa na umri wa miaka 36, alikutwa mauti na polisi mara baada ya kufika katika mji wa Oxford.

Nyumba hiyo ilikuwa na nyoka 140 ndani, jambo ambalo inaaminika kuwa nyumba hiyo ilikuwa maalum kwa ajili ya kuhifadhi wanyama.

Nyoka wapatao 20 wanamilikiwa na bi.Hurst ambaye alikuwa anatembelea mara mbili kwa wiki.

Ingawa nyumba hiyo inadaiwa kuwa inamilikiwa na Benton County Sheriff Don Munson ambaye anaishi nyumba jirani.

Anasema kuwa alimkuta Bi.Hurst kwenye sakafu, gazeti la nchini humo linaripoti.

Aliliambia gazeti kuwa kifo cha bi.Hurst ilikuwa ajali kubwa na amekuwa akionyesha ushirikiano na kila mtu ".

Kamanda polisi katika jimbo la Indiana, Kim Riley anasema kuwa mtu huyo ambaye alimkuta bi.Hurst aliweza kuwaondoa nyoka hao shingoni lakini watu wa dharura walipofika walishindwa kumuokoa.

Bi.Hurst,ambaye alikuwa anaangalia nyoka wake alijeruhiwa na nyoka hao , ingawa ni kitu ambacho alikuwa anakifanya kila wakati bila kudhurika.