Mwimbaji wa muziki nchini, Mimi Mars, ambaye kwa sasa yupo chini ya lebal ya mdee music, ametajwa na tume ya filamu nchini Kenya kuwania tuzo kubwa za filamu (Kalasha International Awards) mwaka 2019.
Mwanamuziki huyo na muigizaji, amechaguliwa kuwania tuzo ya Kalasha awards katika kipengele cha 'Best Actress' katika filamu aliyoigiza na waigizaji kutoka nchini Kenya inayoenda kwa jina la You Again.
Mimi Mars ambaye jina lake halisi ni Marianne Mdee, mdogo wa Vanessa Mdee, aliwahi kuwa mtangazaji na kuhamia katika tasnia ya muziki kwa sasa amejiingiza katika uigizaji huku akifanya vizuri na kuchaguliwa kuwania tuzo ambayo itamtambulisha vyema katika tasnia ya uigizaji.
Aidha, hii ndiyo mara yake ya kwanza kutajwa kama (nominee) kwenye tuzo za filamu.
