TANZIA: Aliyekuwa msanii wa Bongo Fleva Bi Cheka afariki dunia

Msanii mkongwe wa kike wa muziki wa Bongo Fleva, Cheka Hija Mzee, maarufu kwa jina la ‘Bi Cheka’ amefariki dunia mchana huu wa Novemba 28, 2019 katika Hospitali ya Mloganzila, Dar es Salaam.

Kifo cha msanii huyo mkongwe kimethibitishwa na mtoto wake wa kiume, Adam Juma, ambaye amesema kuwa mama yake alikuwa akisumbuliwa na tatizo la moyo.

Familia ya marehemu inaendelea na mipango ya mazishi ambayo itaitangaza.

Bi Cheka atakumbukwa kwa umahiri wake wa ku-rap ambapo aliwahi kufanya kazi nyingi za muziki hasa akiwa na Kundi la TMK. Baadhi ya wasanii aliowahi kufanya nao ngoma ni Mheshimiwa Temba na marehemu Godzilla.