Mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic amethibitisha kuondoka katika klabu ya LA Galaxy ya nchini Marekani aliyojiunga nayo Machi 2018.
Zlatan mwenye umri wa miaka 38 anaondoka LA Galaxy akiwa amecheza mechi 56 na kufunga magoli 52.
“Nilikuja, nikaona, nikateka. Ahsante LA Galaxy kunifanya nijihisi hai tena. Kwa mashabiki wa Galaxy - Mlimtaka Zlatan, nikawapa Zlatan. Karibuni. Stori inaendelea....sasa rudini mkaangalie Baseball” - Aliandika Zlatan katika akaunti yake ya Twita.

