Loading...

12/04/2019

Rais wa Iran asema nchi yake iko tayari kwa mazungumzo ya nyuklia

Rais wa Iran, Hassan Rouhani amesema nchi yake iko tayari kwa mazungumzo ya nyuklia kwa sharti ikiwa Marekani iondoe kwanza vikwazo ''visivyo halali''.

Kauli hiyo ameitoa leo na kurushwa moja kwa moja na televisheni ya taifa. Rouhani amesema kama Marekani imejiandaa kuweka pembeni vikwazo, Iran iko tayari kwa mazungumzo na kujadiliana katika mkutano wa wakuu wa nchi sita zenye nguvu duniani.

Kwa muda mrefu Rouhani amekuwa akiitaka Marekani iondoe vikwazo ili Iran nayo irejee kwenye meza ya mazungumzo.

Mkataba wa kihistoria wa nyuklia uliosainiwa mwaka 2015 uliipa Iran nafuu ya vikwazo vya kiuchumi kwa nchi hiyo kuachana na mpango wake wa nyuklia.

Makubaliano hayo yamekuwa hatarini tangu Rais wa Marekani, Donald Trump alipojiondoa mwezi Mei mwaka uliopita na kuiwekea Iran vikwazo vipya.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger