Na Timothy Itembe Mara.
Diwani kata ya Nkende,Daniel Komote wa Chama cha mapinduzi amewataka viongozi mbalimbali wa kuchaguliwa na wale wakuteuliwa kuwatumikia wananchi kwa lengo la kuwaletea maendeleo.
Komote alitoa kauli hiyo jana mbele ya mkutano wa kata wa kuwasomea wananchi utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama cha mapinduzi 2015-2020 ikiwa ni pamoja na Ahadi alizozitoa wakati akigombea ambazo atekelezea kwa wananchi wake pindi atakapofanikiwa kuchaguliwa katika nafasi hiyo.
" Ndugu zangu wakati nachaguliwa kata ya Nkende kwa ujumla ilikuwa na hali mbaya kimaendeleo lakini baada ya kuchaguliwa nilikaa na viongozi wangu na kupanga mikakati ya kuwaletea wananchi maendeleo ambapo kwasasa Nkende kimaendeleo inaridhisha tofauti na kata zingine hapa nchini"alisema Komote.
Komote aliongeza kuwa kwa miaka (4) ya uongozi wake amefanikiwa kuingiza mpango wa kilomita 97 za miundombinu ya Barabara zilizo sajiliwa na kati ya hizo Kilomita 44 za Barabara zimelimwa ndani ya mitaa yake kumi na Saba na kwa upande wa Elimu kata yake imefanikiwa kusajili wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza wa chaguo la pili mwaka huu.
Upande wa Afya kata ya Nkende tumefanya vizuri ambapo tumefanikiwa kujenga Kituo cha Afya kwa kutumia fedha Milioni 400 tulizoletewa na Serikali pamoja na michango ya wananchi kama vile kutoa eneo la kujenga kituo huku Wananchi wakijitolea mali zaoa na Nguvukazi lengo likiwa ni kufanikisha ujenzi wa kituo cha Afya na kupunguzia wagonjwa kutembea umbali mrefu kwenda kutafuta huduma katika Hospitali ya wilaya taklibani kilomita 16 kwenda na kurudi pindi wanapougua aliongeza kusema Diwani huyo.
Katika mkutano huo Mgeni rasimi Jonadhan Mchango ambaye ni katibu Tarafa Inchage alitumia nafasi hiyo kumpongeza Diwani huyo kuwa kati ya kata alizo na zo ndani ya Tarafa Inchage zaidi 13 diwani Komote anafanya kazi nzuri ya kumsaidia Rais awamu ya Tano John Pombe Magufuli ya kuwatekelezea wananchi maendeleo.
Machango alitumia nafasi hiyo kugawa Kadi za Bima ya Afya zaidi ya 100 na kukamilisha idadi ya wananchama wa Bima ya Afya mfuko wa CHF kata ya Nkende waliounganishwa na diwani huyo kwa kutumia fedha za mfukoni mwake kufikia kaya 410 sawa na Watu 2460 ambapo viongozi wengine walitakiwa kuiga mfano huo wa kuwa na moyo wa kutoa kwani familia zingine ni masikini hazina uwezo wa kujiunga na mfuko wa Afya na kutibiwa pindi wanapokuwa wameugua.
Pia Machango alitumia nafasi hiyo kugawa vifaa vya Ofisi vyenye dhamani ya shilingi Laki Tano vilivyotolewa na Dinwani huyo kwa viongozi mbalimbali wakiwemo wenyeviti wa mitaa yote ya Nkenda,Viongozi wa (5) wa madhehebu ya Dini na viongozi wa matawi ya Chama cha mapinduzi (4) lengo kufanikisha kazi za Ofisi na kuondoa mazingira ya Rushwa baina ya viongozi na wananchi wanaotaka huduma.
Naye mmoja wa viongozi wa madhehebu ya Dini mchungaji Magdalena Alloyce maarufu Mama Weng'ana kutoka kanisa la FPCT Nkongore alipongeza mpango wa diwani kujitolea mali zake na kununua na kuwagawia vifaaa vya Ofisi ikiwemo Rim Paper Moja,File Moja na kalamu 3 za kuandikia kwa kila kiongozi na kutoa huduma Bora kwa Wananchi.
Mwenyekiti wa mtaa wa Kogesenda,Paul Keraryo alisema kuwa kupokea vifaa hivyo vya Ofisi vitaenda kupunguza baadhi ya uhaba na changamoto uliokuwepo na kuwadai wananchi kuleta karatasi za kuandikia huku wananchi wakitafsiri hiyo kuwa ni Rushwa wanazoombwa na kuwa sasa viongozi hao wataenda kuwatumikia wananchi bila kuwadai kalamu na karatasi ili kuwaandikia Barua pindi wanapokuwa wanahitaji.
