Na Paschal Malulu-Kahama
Imeelezwa kuwa jamii wilayani Kahama mkoani Shinyanga inakabiliwa na changamoto ya elimu ya ugonjwa wa kifua kikuu (TB) kutokana na walio na ugonjwa huo kukimbilia kwa waganga wa kienyeji wakidai wamerogwa.
Hayo yamesemwa na mratibu wa magonjwa ya kifua kikuu na Ukimwi halmashauri ya mji wa Kahama Nkoba Luzumbi amesema wananchi hawana uelewa wa ugonjwa huo na pindi anapokuwa ameugua wamekuwa wakikimbilia kwa waganga wa kienyeji na pindi wanapozidiwa na ugonjwa huo unakuwa tayari umekua sugu.
Amesema hali hiyo inasababishwa na jamii kukosa elimu ya kifua kikuu ambapo kwa mwaka 2020 wamejipanga kuwatumia wadau mbalimbali kuhakikisha elimu inawafikia wananchi ili kutokomeza ugonjwa huo ambapo takwimu za mwaka 2019 halmashauri ya mji wa Kahama imepokea wagonjwa 1042 wakiwemo sita walio na kifua kikuu sugu.
Luzumbi amesema kundi jingine ambalo linachangamoto ya kushindwa kutumia dawa ya kifua kikuu ipasavyo ni wachimbaji wadogo kwani wamekuwa wakihama migodi kila kukicha hivyo kwa mwaka huu vile vile wameandaa mpango mkakati wa kuhakikisha wanawasiliana na viongozi wa migodi ili kuendelea kuwahamasisha kutumia dawa.
Amesema migodi midogo inapokuwa inaibuka wachimbaji huwa wanahama bila kujali kama ana dawa au hana kitu ambacho kwa mwaka huu wao kama halmashauri watatumia njia ya kuwaunganisha wamiliki wa migodi hiyo ili wachimbaji wanapohama inakuwa rahisi kuwapata walio katika matumizi ya dawa za ugonjwa huo.
Aidha halmashauri ya mji wa Kahama kwa mwaka 2019 imevuka lengo lililopangiwa na wizara ya afya katika kuibua wagonjwa wa kifua kikuu ambapo walipangiwa kuibua wagonjwa 1001 lakini wamefanikiwa kuibua wagonjwa 1042 sawa na asilimia 104.