IRAN YAHITIMISHA KISASI CHAKE. 

Kiongozi wa juu wa Iran Ali Khamenei amesema mashambulizi hayo ya makombora yalikuwa kibao cha usoni kwa Marekani na kwamba wanajeshi wa Marekani wanapaswa kuondoka katika kanda hiyo.

Alikuwa anahutubia mkusanyiko wa Wairan waliokuwa wanaimba "kifo kwa Marekani".

 Televisheni ya Taifa ya Iran ilisema Iran ilifyatua makombora 15 kuelekea maeneo ya Marekani.

Jeshi la Marekani lilisema maeneo yasiopungua mawili yanayohifadhi wanajeshi wa vikosi vya muungano nchini Iraq yalilengwa majira ya saa saba na nusu usiku, Iraq imesema makombora 22 yalifyatuliwa.

 Maafisa wa Iran wamesema Tehran haikutaka vita na mashambulizi yake yamehitimisha majibu yake kwa mauaji ya Qassem siku ya Ijumaa, jenerali ambaye mazishi yake baada ya siku kadhaa za maombolezi yalifanyika wakati makombora hayo yalipofyatuliwa. Televisheni ya Iran iliwaonesha waombolezaji wakishangilia.