JPM awaapisha Mabalozi awaJPM awaagiza kufanya kazi

Rais John Magufuli leo Jumanne Januari 14, Ikulu jijini Dar es Salaam amewaapisha mabalozi wateule wanne, ambao ni Meja Jenerali Mstaafu Gaudence Milanzi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Dk. Modestus Kipilimba kuwa Balozi wa Tanzania nchini Namibia, Profesa Emmanuel Mbennah kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe na Dk. Benson Bana kuwa Balozi Tanzania nchini Nigeria.

Rais Magufuli amewaagiza mabalozi hao kusimamia uchumi na kuhakikisha wanatengeneza ajira kwa watanzaniakatika nchi wanazoziwakilisha  na kuwataka kufanya kazi kwa mujibu wa sheria ya nchi.

“Mabalozi mliapishwa leo ninaamini mnakwenda kufanya majukumu yenu kwa faida ya nchi yetu kwani kila nchi mlizopangiwa zina umuhimu wake na mnafahamu mikakati tuliyo nayo ndani ya SADC katika kujenga maendeleo na uchumi wa kisasa,” – JPM


“Tunataka unapoteuliwa ukachape kazi kwani hii ndio maana ya ule usemi wa hapa kazi tu na nina uhakika mtaweza tu hivyo nendeni katika maeneo yenu mliyopangiwa mkiamini kwamba mnawakilisha taifa lenye mwelekeo mpya katika maendeleo ya watu wake,” – JPM
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia