Kiongozi wa jeshi la Iran atishia kuteketeza maeneo yanayopata msaada kutoka Marekani

Kiongozi wa jeshi la mapinduzi la Iran, Hossein Salami, ametishia leo kuteketeza maeneo yanayopata msaada kutoka Marekani kufuatia kuuwawa kwa jenerali wa ngazi ya juu wa Iran katika shambulio la anga la Marekani wiki iliyopita Salami alitoa ahadi hiyo mbele ya kundi kubwa la maelfu ya watu waliokusanyika katika uwanja wa kati katika mji wa Kerman, mji alikozaliwa marehemu Jenerali Qassem Soleimani, aliyeuawa na Marekani.

Ahadi yake inaakisi madai ya maafisa wa ngazi ya juu wa Iran, kuanzia kiongozi mkuu wa taifa hilo Ayatollah Ali Khamenei na wengine, pamoja na waungaji mkono nchini humo, wakitaka kulipiza kisasi dhidi ya Marekani kwa mauaji hayo ambayo yamepandisha kwa kiasi kikubwa hali ya wasi wasi katika eneo la Mashariki ya Kati.
Mpya zaidi Nzee zaidi