Madiwani halmashauri ya Tarime vijijini wagomea vikao viwili kwa siku moja

Na Timothy Itembe Mara.


JITIHADA za Mkurugenzi wa halmashauri ya Tarime vijijini za kutaka  kikao cha Baraza la kujadili na kupitisha Rasimu ya Bajeti 2020/2021 pamoja  na Mapitio ya Bajeti 2018/2019 kifanyike kwa siku moja badala ya siku mbili kama ilkivyo zoeleka zimegonga mwamba baada ya Madiwani kumgomea.

Madiwani hao kwa pamoja waliamua kwa kupiga kura ya wengi wape na kuwa mkutano wa Baraza wa mapitio ya bajeti 2018/2019 ufanyike siku moja na ule mkutano wa Barza la kujadili na kupitisha rasimu ya Bajeti 2020/2021 ufanyike siku nyingine tofauto badala ya ilivyokuwa umepangwa na mkurugenzi wa halmashauri hiyo,Apol Tindwa ambaye hakuwepo kikaoni kwa madai kuwa alikuwa naudhuru mkutano huo ufanyike kwa siku moja

Baada ya majadaliano marefu ya madiwani na kaimu mkurugenzi halmashauri ya Tarime vijijini,Slevanus Gwiboha alyekuwepo hapo jana kwenye kikao na kutoa maelezo marefu juu ya  jitihada  kwanini wanataka mkutano wa jana wa madiwani wa  baraza la kujadili na kupitisha rasimu ya Bajeti,2020,2021 na ule wa kujadili mpango wa mapitio ya Bajeti,2018/2019 ufanyike  kwa siku moja badala ya bili kama ilivyo kwenye kanununi  ya halmashauri Namba Tano kuwa ni  uharaka wa kuwahi mda  jitihada hizo bado ziligonga mwamba kwa madai kuwa kura imepigwa na wengi wamesema kikao kifanyike kwa siku mbili kama ilivyo kawaida badala ya moja iliyokuwa imepangwa.

Diwani kata ya Regicheri.John Bosco kutoka chama cha mapinduzi alisema kuwa kura ikipigwa imefunga mjadala  na imekuwa sheria vinginevyo mwenyekiti wa siku hiyo Nyangoko Paull kuendelea kuruhusu mjadala tena hali kura imepita nikukiuka Taratibu zilizowekwa na kupitishwa.

Kaimu mkurugenzi wa siku hiyo,Slyevanus Gwiboha licha ya kujitahidi kufanyike kikao kwa siku mbili na hoja yake kupingwa na kura aliwapongeza madiwani hao kuwa uwamuzi waliouchukua wa kupiga kura kwa kukoti kanuni ya halmashauri na kupitisha kikao kifanyike siku mbili badala ya moja niwakidemokorasia.

Baada ya marumbano marefu na kura kuamua kikao cha Mpango wa Rasimu ya Bajeti 2020/2021  kuhairishwa na kupangwa kufanyika siku  nyingine madiwani kwa pamoja waliridhia kifanyike  kikao cha Mapitio ya Bajeti 2018/2019 hapo jana ambacho kilifanyikia  katika ukumbi wa shule ya Sekondari JK Nyerere iliyopo Nyamwaga ambapo kilifanyika na hoja zikaendelea.




Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items