Na James Timber, Mwanza
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limefanikiwa kuwakamata watu saba kwa tuhuma za kujifanya maofisa usalama wa Taifa kutoka Ikulu, ambao wamekuwa wakiwatapeli wananchi na baadhi ya watumishi wa serikali katika Jiji la Mwanza.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza ACP Muliro Muliro, amesema matukio hayo yametokea kati ya Desemba 27, mwaka jana na Januari 2, mwaka huu, Nyakato wilayani Nyamagana, walipokuwa wanatumia gari lenye NA. T.751 BNL, aina ya Toyota Ambulance, ambalo walidai ni sehemu ya msafara wa viongozi wakuu.
Kamanda aliwataja Watuhumiwa waliokamatwa ni Chalanga Chalanga (45) Mkazi wa Pasiansi na Arusha Hamis Mwalimu (25) Fundi magari, kujifanya bodygurd wà Chalanga Chalanga, Philipo Petro (35), Mkazi wa Usagara Misungwi, pia dereva wa Chalanga Chalanga, Elia Gunda (30) anayedai yeye ni mchungaji wa Kanisa la EAGT liliopo Kisesa pia Mkazi wa Kisesa. Hassan Juma (29) Mkazi wa Mkolani Fundi wa IT, Seleman Karanga (25), anajifanya Mlinzi Mkuu wa Chalanga Chalanga na Afisa Mkuu wa Ikulu Michael Mazige Mkazi wa Morogoro.
"Tumemkamata tapeli ambaye alikuwa anawapigia watu simu na kujifanya kuwa yeye ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, amefahamika kwa jina la Ashery Justol (30) Mfipa Mkazi wa Igoma Mwanza, kabla ya kukamatwa alikuwa akiwapigia simu watu na kuwatumia ujumbe mfupi na kuwaeleza amepatwa matatizo ya kijamii na kuwataka washiriki kwa kumchangia fedha au vitu," alisema.
Aidha mtuhumiwa huyo alichukua Picha ya Kamanda na Kamanda Muliro Muliro kwenye mtandao yenye sare za Jeshi la Polisi na kuiweka kwenye Profile yake ya WhatsApp kisha kutumia mtandao huo kuwasiliana na watu kwa lengo la kuwatapeli.