Loading...

1/14/2020

Marekani yadai shambulizi lililofanywa na Msaudia lilikuwa la kigaidi

Wachunguzi nchini Marekani wamesema shambulizi lililofanywa na afisa wa jeshi la Saudi Arabia kwenye kituo cha jeshi la wanamaji la Marekani jimboni Florida Desemba iliyopita, lilikuwa la kigaidi.

Waziri wa Sheria wa Marekani William Barr amesema afisa huyo alikuwa amechapisha kauli za chuki dhidi ya Marekani na Israel katika mitandao ya kijamii, na alikuwa amesifu hujuma za kigaidi.

Barr amesema haielekei mshambuliaji huyo aliyeuawa baada ya kuwauwa wanajeshi watatu wa Marekani, hakuwa na washirika.

Hata hivyo, Saudi Arabia itawarejesha nyumbani maafisa wake wengine 21 waliokuwa wakipata mafunzo katika kituo hicho, baada ya wachunguzi kusema walikutwa na mafaili ya kigaidi na ya ngono inayowahusisha watoto.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger