Moto wateketeza jengo la ghorofa tatu

Na James Timber, Mwanza



Jengo lenye ghorofa tatu liliopo maeneo ya Isamilo katika wilaya ya Nyamagana mkoani hapa, limeteketea kwa moto Majira kati ya saa 12 jioni, huku chanzo kikiwa hakijajulikana.

Hata hivyo hadi kufifia kwa moto huo hakuna mtu yeyote  anayeripotiwa kuathirika na moto huo, huku baadhi ya mashuhuda wakazi wa jirani wa jengo hilo wamesema kuwa zimamoto walifika mapema na kusubiri TANESCO, jambo lilopelekea kuongezeka kwa moto huo.

Mpya zaidi Nzee zaidi