Uturuki yaanza kupeleka wanajeshi Libya

Raisi wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema nchi yake imeanza kuwapeleka wanajeshi wake Libya, ili kuisaidia serikali ya Waziri Mkuu Fayez al Serraj inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa.

Rais Erdogan ameyasema hayo leo Alhamisi ikiwa zimebaki siku chache kabla ya mkutano wa Berlin, utakaojadili mgogoro wa Libya .

Wiki iliyopita, Uturuki na Urusi zilizitaka pande zinazohasimiana za nchini Libya kutia saini makubaliano ya kusitisha mapigano.

Mazungumzo hayo yaliyofanyika mjini Moscow yalikuwa na kusudi la kusimamisha kampeni ya muda mrefu ya Jenerali muasi Khalifa Haftar ya kutaka kuudhibiti mji mkuu wa Libya, Tripoli hata hivyo pande hizo mbili hazikufikia makubaliano baada ya Jenerali Haftar kuondoka bila kutia saini mkataba huo.