Babati: Mbwa wanaozurura Ovyo kwenye Mitaa Kupigwa Risasi

Na John Walter-Babati-Manyara

Mbwa wanaozurura ovyo katika mji wa Babati mkoani Manyara wameanza kuangamizwa kwa kupigwa risasi kwa amri ya mkurugenzi wa mji wa Babati Fortunatus Fwema.

Amesema wamechukua uamuzi wa kuwaua  kufuatia ongezeko kubwa la Mbwa wanaozurura mitaani na kutishia usalama wa Wakazi wa mji huo.
Mkurugenzi huyo amesema zoezi hilo limeanza leo Februari 13,2020 na litaendelea katika maeneo yote ya Mji wa Babati hivyo wananchi wanaofuga mbwa wahakikishe kuwa wanawafungia ndani.

Afisa Mifugo wa mji wa Babati Godfrey Mrema amesema wanaua mbwa wanaowakuta wanazurura mtaani.

Amewataka Wananchi wazingatie sheria za kufuga mbwa kwa kuwafungia klwenye mabanda au cheni na kuwafungulia kuanzia saa kumi na mbili jioni.

Baadhi ya wananchi wameunga mkono hatua hiyo kwa kueleza kuwa wakimalizika watabaki salama kwa kuwa wamekuwa wakipata vitisho vya mbwa hao.

Inaelezwa kwamba kipindi cha kuanzia Junuari 2017 hadi mwishoni mwa Mei 2017  jumla ya watu 264 waling’atwa na Mbwa.
Kwa mujibu wa sensa ya mifugo ya mwaka 2016 mji wa Babati unakadiriwa kuwa na Mbwa 4,923 ambao kati yao Mbwa 3,693 sawa na asilimia 75 wanazurura mitaani ambapo asilimia 35 ya mbwa hao wanaozurura  hawana wamiliki.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia