Jinsi ya kuongeza ufanisi katika kazi yako

Wakati mwingine ili uweze kuwa bora kwenye kazi unayoifanya basi unatakiwa kuelewa vyema namna ambavyo utaweza kuwa bora katika kazi hiyo  unayoifanya hatimaye upate matokeo yenye thamani mbele yako na watu wengine kwa ujumla.

Mara nyingi huwezi kusema unataka mafanikio katika kile ukifanyacho wakati huo  huo umesahau kufanya mambo ya msingi yatayokusaidia kuwa hivyo. Kila wakati unatakiwa kuelewa ubora na uzuri wa kitu huwa unatengenezwa na muhusika wa kitu hicho.

Hivyo iwe umejiari au umejiriwa basi unatakiwa kuzingatika mambo ya muhimu ambayo nitakueleza katika makala haya namna ambavyo unaweza kuongeza ufanisi wa kiutendaji katika kazi zako kama ifuatavyo;

Ili uweze kuwa bora na kuongeza ufanisi katika kazi yako unayoifanya basi unatakiwa  kujitambua mwenyewe. Katika suala la kujitambua wewe binafsi ni lazima ukae chini na kutafakari kuhusu mstakabali mzima wa maisha yako.

Unapofanya tafakari kuhusu wewe, unatakiwa kujua wewe ni nani? unataka kufanya nini na kwa muda gani? Na unataka kufanikiwa kwenye eneo gani hasa?. Vile vile ni lazima uelewe kusudio la kuumbwa kwako.

Kila mwanadamu ameubwa kwa kusudio lake hapa dunia hivyo ni lazima mtu huyo aweze kutumikia hilo kusudio lake, kama ni kipaji basi unatakiwa kikutumia vyema hivho kipaji, kama ni biashara basi unatakiwa kuifanya vyema.

Kila wakati unatakiwa kujihoji maswali muhimu ambayo yatakusaidia sana kuweza kujitambua wewe mwenyewe, kwa kila swali ambalo utakuwa unajihoji unatakiwa kutafuta majibu sahihi ya maswali hayo.

Unatakiwa kufanya hivyo kwa sababu watu wengi tumekuwa tukiishi maisha ya ukawaida sana au kwa maneno mengine maisha ya kimazoea na ndiyo maana hata matokeo ya vitu tunavyovifanya vimekuwa vikileta  matakoe kawaida pia.

Hivyo ili kuepukana kupata matokeo ya kawaida kwenye vitu tunavyofanya tunakiwa kuwekeza muda mwingi katika  kujitambua sisi mwenyewe kwa kuangalia malengo yetu na kazi ujumla.

Vile vile ili uweze kupata matokeo chanya kwenye kazi unayoifanya basi uanatakiwa kufanya kitu cha tofauti. Katika dunia hii karibia asilimia 50 ya vitu vinavyofanywa na mwanadamu ni kwamba vitu hivyo vinafanana, Hivyo ili kupata matokeo tofauti na watu wengine basi uanatakiwa kuongeza thamani zaidi katika kitu hicho ili kujitofautisha na watu wengine.

Kwa mfano kama unauzaa mchele fahamu kila mtu naye anafanya biashara hiyo ya kuuza mchele, swali la kujiuliza ni je unajitofautishaje na watu wengine wanaofanya biashara kama yako?

Kila wakati ili uweze kuongezea thamani katika kazi basi unatakiwa kuelewa namna ambayo utajitofautisha wewe na watu wengine wanaofanya kitu kinachofanana na wewe.

Lakini mbinu nyingine ambayo itakufanya uongeze ufanisi wa kiutendaji katika kazi unayoifanya ni kutafuta muda wa kufanya kitu kimoja kwa umakini kazi unayoifanya. Kwa mfano kwa siku tunayo masaa 24 hivyo inatakiwa masaa mawili tu ya kufanya kitu cha maana.

Masaa haya mawili kwa kitaalum huitwa  na masaa ya dhahabu, yaani muhusika anatakiwa kuweka nguvu nyingi za umakini katika kufanya kazi katika masaa hayo. Pia katika masaa hayo mawili unatakiwa kuelewa kwamba mawazo yako yanatakiwa kutulia katika kufikiri na kufanya kazi kwa umakini wa hali ya juu sana ili kupata matokeo chanya katika kazi hiyo unayoifanya.

Ukiyazingatia hayo mambo muhimu niliyokujuza siku ya leo katika makala haya basi maisha yako yatabadilika kwa kiasi kikubwa sana.