Mambo ya kufanya ili uweze kuondokana na tabia ya kutokutekeleza malengo


Wataalamu wa maswala ya sayansi wanabainisha kuwa,tabia tunazoishi leo ni matokeo ya yale tuliyojifunza katika umri wa kuanzia miaka 0-7. Kipindi hicho ndicho kilichomtengeneza mtu unaemwona leo. Huhitaji kuhangaika sana ukikutana na mtu ambaye ana tabia fulani rudi nyuma ujifunze mizizi yake utotoni alikuwaje.

Ubongo wa mtoto mdogo ni kama shamba zuri tupu lenye udongo wenye rutuba nyingi ambayo iko tayari kukuza mbegu yoyote utakayokwenda kupanda. Ukipanda mbegu mbaya itaota na kukua na matunda kuonekana kadhalika hata ukipanda mbegu nzuri pia.

Wataalam wa maswala ya sayansi ya ubongo wa wanabainisha kuwa akili ya binadamu ili ifanye kazi imegawanyika katika sehemu mbili muhimu. Conscious mind na subconscious mind. Conscious mind inasemekana yenyewe inachukua 5% tu ya akili wakati 95% yote ni subconscious mind.

Kutokana na uwiano huo hapo juu utabaini kuwa subconscious mind ina nguvu sana, kwa hiyo katika maisha yetu maamuzi mengi tunayofanya tunaongozwa na sehemu hii. Ingawa sijapata Kiswahili chake lakini sub ni chini ya au ya chini.

Kazi ya consciuos mind huwa ni kufanya maamuzi muhimu yote kwa umakini matukio yote ya ubunifu hufanywa katika eneo hili. Kupitia conscious mind ndipo mtu huweza kujitambulisha yeye ni nani na subconscious mind ambayo huongozwa na hisia yenyewe hutunza kumbumbu za matukio yote ambayo umepitia katika kipindi chote cha maisha yako tangu utoto.

Wakati unazaliwa ulikuwa na tabia na imani ziro hukuzaliwa na chochote ulikua mweupe kabisa. Kwa hiyo katika kipindi chote cha miaka 7 ya mwanzo, ubongo wa mtoto ambao huwa kama karatasi ambayo haijaandikwa hujifunza kwa kukusanya taarifa zote na kutunza kwa ajili ya matumizi ya muda mrefu maisha yake yote. Tabia uliyo nayo ulijifunza katika kipindi hicho cha utoto kutoka kwa wazazi wako na watu waliokuzunguka (jamii).

Ni kutokana na imani hiyo ambayo tulijifunza bila kujua katika kipindi muhimu cha utoto ndio maana utakuta waliofanikiwa wataendelea kufanikiwa na wale wasiofanikiwa wataendelea kubaki bila kufanikiwa. Tajiri watakuwa tajiri na masikini watakuwa masikini mpaka kufa.

Tangu wakiwa wadogo waliambiwa kuwa huwezi kufanikiwa kwa vyovyote kama unatoka familia maskini. Kwamba huwezi kufanikiwa katika maisha mpaka uwe na cheti kizuri cha shule. Uongo mwingi ambao tuliaminishwa tukiwa wadogo umegeuka kuwa imani ambayo tunaishi nayo kwa uchungu.

Uongo huo umeleta matatizo makubwa katika maeneo mbalimbali ya maisha yetu. Mahusiano na watu wengine mahali pa kazi,katika kampuni,mashirika yameharibika,mafanikio yetu yamedumaa,tumeshindwa kabisa kufikia malengo yetu.

Bila shaka utakubaliana nami kuwa watu wengi katika sehemu hii wamekwama japokuwa unaona wanaishi na wanafanya mambo,ukweli ni kwamba wanafanya chini ya kiwango au uwezo wao kwani wangeweza kufanya zaidi ya hapo.

Yafuatayo ni mambo ya kufanya ili uweze kuondokana na tabia ya kutokutekeleza malengo;

Tambua eneo ambalo linakusumbua.
Umehangaika kwa miaka mingi sasa unataka kujiondoa kwenye tabia ambayo huipendi kwa sababu haikusaidii; hatua ya kwanza unapaswa kubainisha tabia ambayo unataka kuifukuza il uweze kukaribisha tabia mpya katika maisha yako na uanze kuishi maisha ya mafanikio.Kumbuka hakuna nafasi ya tabia mbili kukaa pamoja lazima moja itoke ili iingie nyingine.

Hatua hii itakusaidia kuanza sasa mchakato wa kujitoa kwenye tabia au tatizo hilo kwani huwezi kamwe kujitoa kwenye kitu ambacho hata hujui ni tatizo gani linalokusumbua!  Ni kama vile ukinunua komputa iliyotumika ili ikusaidie kwanza unaondoa program zote usizozitaka na kuweka zile ambazo unazitaka kulingana na mahitaji yako.

Jifunze kutoka kwenye tabia hiyo usiyoitaka
Kabla hujajifunza tabia mpya unayotaka kuhamia katika eneo fulani, hatua ya kwanza unapaswa kuhama kwanza unlearn au kuondoa tabia ambazo umejifunza zamani ili uweze kuweka tabia mpya. Huwezi kujifunza tabia mpya wakati bado umeshikilia ile ya zamani.Tabia ya zamani itoke izibwe na tabia mpya.

Unafanyaje sasa? Unakumbuka zile pande mbili za ubongo unavyofanya kazi conscious mind na subconscious mind? Hapa unapaswa kushughulika na subconsiuos mind kuifundisha kuwa unahama kutoka tabia hii kwenda tabia nyingine.

Tuseme labda una ugonjwa wa kutokutumia muda wako vizuri. Hakuna mahali unawahi kwa wakati kila unapoalikwa kwenda kwenye jambo lolote lazima uwe wa mwisho mpaka watu wanajua kuwa hiyo ni sehemu ya udhaifu na tabia yako. Unachopaswa kufanya ni kujiambia “katika swala la muda nimebadilika”. Inaweza kuwa asubuhi mchana na jioni au katika kipindi chochote utakachochagua mwenyewe fanya hivyo.

Jiambie hivyo kila unapokumbuka na kuamini moyoni mwako kwamba jambo hilo limekwishawezekana huku maneno yako yakisindikizwa na matendo yanayokusaidia sasa kuvuka kutoka upande huu kwenda upande mwingine.Kama ulikuwa unachelewa kwenye mialiko sasa jitahidi kujifunza kuwahi. Itaweza kuwa shida siku za mwanzoni lakini kadri unavyo kwenda ndivyo subconsciuos mind inavyozoea jambo hilo la kuwahi na kuwa sehemu ya tabia yake sasa.

Uende taratibu huku ukiwa unajua kuwa ndani mwako kunaweza kuwa na upinzani unaoweza kukufanya ushindwe kutimiza azma yako ya kuwa meneja wa muda wako mwenyewe kwa sababu siyo tabia uliyozoea lakini hilo ni swala la muda tu.  Kwa nini upinzani? Ni kwa sababu kazi kubwa ya akili (subconscious mind) ni usalama wako kwanza. Inajipanga kukukinga na hatari yoyote ambayo inaona kutokana na kumbukumbu za matukio ya nyuma uliyoona,uliyosikia ilik kukukwepesha hatari.

Rudia rudia kwa matendo mpaka ujitoe
Wakati mtoto mdogo wa umri kati ya miaka 0-7 hujifunza kwa kutazama wazazi wake na jamii inayomzunguka ili kuweza kujua namna ya kuishi katika jamii,njia nyingine ya watu wazima kujifunza ni kurudia rudia mpaka inakuwa tabia mpya. Mfano kama tabia yao ni kuchelewa katika kila tukio basi sasa anza kuwahi angalau dakika 10 kabla ya tukio fanya hivyo kwa kurudia mara saba na kuendendelea utajikuta unafanikiwa toka huko usikokutaka.

Kuna msemo wa kiingereza unaosema “repitation is power” Kurudia ni nguvu.Sababu ya kurudia rudia ni kuifundisha subconscious mind yako tabia mpya unayoitaka na kwa kufanya hivyo upinzani kutoka kwa subconscious mind utaendelea kupungua na mwisho itaidaka na kuanza kufanya kuwa tabia ambayo sasa hausumbuki tena kufanya kwa sababu imeizoea.Kumbuka ukishafika hatua hiyo sasa usipowahi subcosciuos mind itadai.

Hivyo ndivyo unavyoweza kufanya mabadiliko katika maeneo mbalimbali ya maisha yako iwe mahusiano,afya,uchumi n.k na kujikuta unafanikiwa katika maeneo mengi ikiwemo kutekeleza malengo unayojiwekea mwenyewe. Naamini makala hii itagusogeza  hadi mahali fulani na kama ndivyo naomba umsaidie mtu mwingine kama wewe.

Naamini utakuwa umepata kitu kingine kupitia makala hii fupi. Ukiwa na uhitaji wowote au ushauri katika eneo lolote la kuboresha maisha yako usisite kuwasiliana nasi kupitia njia za mawasiliano hapo chini.Aidha kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno au whatsapp au piga simu au email tutapokea na kurudi kwako mapema kadri itakavyowezekana.