Njombe: Wananchi walia na wezi wanaotuhumiwa kutumia ushirikina ili kupotea



Na Amiri kilagalila,Njombe

Wakazi zaidi ya 1600 wa kijiji cha Utalingolo halmashauri ya mji wa Njombe wamelazimika kukutana kwa dharula kuwekeana mikakati ya kukabiliana na wimbi la wizi na ujambazi wa ajabu ulioibuka kijijini hapo ambao unahusishwa na imani za kishirikiana .

Wakazi hao wamesema watekelezaji wa matukio hayo wanaziba sura na kisha kuvamia majumbani usiku na mchana huku wakiwa na siraha wakitaka kupewa vitu vya thamani na fedha na kisha kutokomea kama mizuka.

Kutokana na hali hiyo serikali ya kijiji imelazimika kuunda kamati yenye watu kutoka makundi mbalimbali katika jamii wakiwemo wazee pamoja vikundi vya vijana 10 kila kitongoji ambao wanakwenda kuanza operesheni ya kuwasaka wahusika wa uhalifu huo

Anna Poul na Felis Msigwa ambao ni wananchi wa kijiji hicho wanasema wanahisi watu hao wanatumia nguvu za giza kutekeleza matukio hayo kwani wakishatenda uhalifu wanatoweka katika mazingira yakutatanisha.

"Kuna wizi mwingine ni waajabu,utakuta mnafika kwenye tukio mnazingira nyumba lakini mwizi haonekani,kwa kweli kijiji hiki kimepatwa na majanga makubwa maana wanavunja kwa kutumia mapanga na vitu vingine tunavyokuwa tunasogea kwenye eneo waliloiba matokeo yake hatumpati mtu"alisema Felis Msigwa

Akiweka bayana maazimio yaliofikiwa mtendaji wa kata ya Utalingolo Atanasio Thomas anasema mbali na suala la usalama katika mkutano huo wananchi wamekuliana kuanzisha kamati za maadili ambazo zinakwenda kushughulika na vijana wanaovalia milegezo,wacheza kamali pamoja na unyoaji usio na maadili kwani ndiyo chanzo cha yote.

"Ni kweli hili wimbi limekuwa kubwa, hasa hasa kijiji cha Utalingolo sasa wameunda kamati ya maadili kwa kila kitongoji wameweka watu wawili ambao watadili na kurekebisha tabia za vijana"alisema Atanasio Thomas

Petro Mahenge ni moja kati ya vijana wengi waliojumuishwa kwenye kikosi cha ulinzi shirikishi ambacho kinakwenda kupewa mafunzo ya usalama ili kuanza kazi amesema watatumia kila mbinu kuwanasa wahalifu na kurejesha amani kijijini kwao.

"Kufuatana na mkutano tuliokuwa nao leo zaidi ya wananchi 1600 wamebariki kurudia ile sungusungu ya zamani tuiboreshe zaidi ili kukabiliana na wezi"