Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) imesema itahakikisha inafanya jitihada za za kuimarisha ukuaji wa Chuo cha Usimamizi Wanyamapori (Mweka) kwa kuunganisha wafadhili mbalimbali ili kuboresha zaidi utoaji wa taaluma hiyo muhimu hapa nchini.
Ameyasema hayo Ofisa Mwanadamizi programu ya Maliasili kutoka SADC ,Debora Kahatano wakati alipotembelea chuo cha Mweka kwa ajili ya kuangalia muenendo wa chuo pamoja na kujadili njia bora za kuimarisha hadhi ya chuo hicho.
Pua amesema,SADC inatambua mchango wa chuo hicho kwani kimekua mahiri katika utoaji wa taaluma ya uhifadhi ya wanyamapori tangu kilipoanzishwa mwaka 1963 na kutoa mafunzo kwa nchi za Jumuiya hiyo.
Masururi Beka ni mkuu wa idara ya utalii katika chuo hicho ambapo amesema kuwa ujio wa SADC katika chuo hicho utaleta ushirikiano mwingine utakao kifanya chuo hicho kuendelea kuwa kituo bora cha umahiri wa usimamizi na uhifadhi wa wanyamapori.
Amesema chuo hicho kilipoanza kilikuwa na wanafunzi 25 pekee mwaka 1963 ambapo mpaka sasa chuo hicho kina jumla ya wanafunzi 850 na kusema kuwa ongezeko hilo linahitaji madarasa ya kutosha na magari kwa ajili ya kwenda kwenye mafunzo