Idadi ya vifo kutokana na virusi vipya vya corona imepanda kwa kasi leo baada ya maafisa kubadilisha mbinu zao za kuhesabu, na kuzusha wasiwasi kuwa janga hilo ni baya hata zaidi kuliko linavyoripotiwa.
Wakati idadi ya visa ikiongezeka nchini China, watu 10,000 wamewekwa katika karantini katika nchi jirani Vietnam baada ya visa sita kugunduliwa kwenye vijiji kadhaa, ikiwa ni mara ya kwanza kwa hatua kama hiyo kuchukuliwa nje ya China.
Chini ya shinikizo kutoka nyumbani kuhusiana na namna inavyoushughulikia mzozo huo wa kiafya, Chama cha Kikomunisti cha China kimewafuta maafisa wawili waandamizi katika mkoa wa Hubei, ambao ndio kitovu cha mripuko huo.
Hatua hiyo imekuja saa kadhaa baada ya Rais Xi Jinping kudai kuwa kuna matokeo chanya katika juhudi za kulidhibiti janga hilo ambalo sasa limewauwa zaidi ya watu 1,355.
Watu 60,000 wameambukizwa virusi hivyo. Lakini Shirika la Afya Ulimwenguni - WHO limesema ni mapema mno kutangaza ushindi.