Umoja wa Mataifa wapitisha azimio kuhusu chanjo ya virusi vya corona

MIAKA 73 YA UMOJA WA MATAIFA: | Gazeti la Rai

Mataifa 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa yamepitisha azimio linalohimiza kuwepo usawa kwa kila nchi duniani kupata chanjo ya virusi vya corona itakayopatikana katika juhudi zinazoendelea.

Azimio hilo ambalo lilitayarishwa na Mexico na kuungwa mkono na Marekani linatoa wito pindi chanjo itapatikana mataifa yote ulimwenguni yanapaswa kuipata kwa usawa, kwa wakati na kwa kiwango kinachotosheleza.

Azimio hilo limefikiwa wakati ulimwengu unazidisha kasi ya kutafuta tiba na chanjo dhidi ya virusi vya corona ambavyo vimeshawakumba kiasi watu milioni 2.4 kote duniani na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 165,000.

Kadhilika kupitia azimio hilo, wanachama wa Umoja wa Mataifa pia wamesifu nafasi muhimu iliyochukuliwa na shirika la afya duniani WHO katika kuongoza vita dhidi ya janga la Corona licha ya ukosoaji kutoka Marekani.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia