Chuo kikuu cha Oxford kufanya majaribio ya chanjo ya Covid-19 Kenya


Kulinagana na taarifa zilzitolewa ni kwamba chuo kikuu cha Oxford  kipo mbioni  kufaanikisha chanjo  dhidi  ya virusi vya corona na kutaraji kuifanyia majaribio nchini Kenya kwa watu wazima.

Taarifa hizo zinaendelea kufahamisha kuwa chanjo hiyo itatolewa kwa watu wenye umri wa zaidi ya miaka  18 nchini Kenya kwa watu wasiopungua 400.

Wauguzi na madakatari bingwa ndio watakaoshirika katika kampeni hiyo ya kuoa chanjo  hiyo ambayo itatolewa kwa watu wazima ambao watajitolea.

Chanjo hiyo itaendeshwa katika  mjini wa Kilifi na Mombasa , miji ambayo  imetanjwa kuwa na virusi vya corona  vinaendelea kuzagaa.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alifahamisha mwezi uliopita kuwa raia wa Kenya hawawezi kutumiwa kwa kujaribu chanjo ya aina yeyote.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia