Ifahamu Hospitali iliyozalisha watoto zaidi ya 100, Kutoka kwa wanawake wenye Corona



Watatu kati ya watoto 115 walizaliwa kwa akinamama wenye virusi katika hospitali kuu ya Manispaa ya Lokmanya Tilak  – katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita ,awali walipatikana na Covid-19, lakini vipimo vya madaktari vilionyesha kuwa hawakua na virusi, wamesema madaktari.

Wanawake wengine wawili wajawazito walifariki dunia hospitalini, mkiwemo mmoja ambaye alikufa kabla ya mtoto wake kuzaliwa.

Huku ukiwa na watu takriban 24,000 walioripotiwa kuambukizwa corona na zaidi ya vifo 840 hadi sasa, mji mkuu wa biashara na burudani wa Mumbai umekua ni kitovu cha Covid-19.

Zaidi ya nusu ya watoto walizaliwa kwa wanawake walioathiriwa hospitalini -pia katika hospitali ya Sion – walizaliwa kwa njia ya upasuaji, huku waliosalia wakizaliwa kwa njia ya kawaida, walisema maafisa.

Hamsini na sita kati yao walikua ni wa kiume, huku 59 wakiwa ni wa kike. Ishirini na wawili kati ya wakinamama hawa waliletwa kutoka katika hospitali nyingine : Haijawa wazi ikiwa wengi wa wanawake hawa walipata maambukizi nyumbani, sehemu nyingine au hospitalini.

Timu ya madaktari 65 na wauguzi 24 wamekua wakiwatibu wanawake walioambukizwa corona katika vitanda 40 maalumu. Huku kukiwa na idadi kubwa ya maambukizi , hospitali inapanga kuongeza vitanda vingine 34 kwa ajili ya wanawake wajawazito wenye maambukizi ya Covid-19.

Wanawake hao walijifungulia kwenye vitanda 6 vya kujifungulia katika vyumba vitatu vya upasuaji na wauguzi na madaktari wa nusu kaputi wanatumia mavazi ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya corona.

“Tunabahati kuwa wengi miongoni mwa wanawake waliopatwa na maambukizi kwa sasa hawaonyeshi dalili yoyote kabisa ya virusi vya corona. Baadhi yao walikua na homa na waliripoti kukosa pumzi. Tumewatibu na kuwaruhusu waende nyumbani baada ya kujifungua ,” Dr Arun Nayak, mkuu wa kitengo cha wanawake katika hospitali, amesema


Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia