Jumuiya ya wafanyakazi wa afya nchini Indonesia imesema leo hospitali kwenye mji wa pili kwa ukubwa nchini humo wa Surabaya zimezidiwa na wimbi jipya la visa vya virusi vya corona na zinalazimika kukataa kuwapokea wengine.
Hospitali mbili za mji huo zilizotengwa kuwatibu wagonjwa wa COVID-19 zimefurika wagonjwa huku kukiwa na wasiwasi kuwa janga hilo linasambaa kwa kasi kutoka mji mkuu Jakarta kuelekea maeneo mengine ya Indonesia.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyakazi wa afya katika jimbo uliko mji wa Surabaya amesema wanashuhudia ongezeko kubwa la wagonjwa kuzidi idadi ya vitanda vilivyo hospitali.
Tangu Mei Mosi idadi ya visa vya COVID-19 kwenye jimbo la Java Mashariki imepanda kwa asilimia 300 na kufikia wagonjwa 4,313 leo Alhamisi tofauti na ongezeko la asilimia 60 pekee katika mji mkuu Jakarta.