Iraq itaweka hatua ya kufunga shughuli zote na kuzuia watu kutoka nje katika baadhi ya maeneo ya mji mkuu Baghadad.
Waziri mpya wa afya nchini humo ameeleza hayo leo katika wakati ambapo visa vya maaambukizi ya virusi vya corona vimeongezeka katika kipindi cha wiki kadhaa tangu vizuizi dhidi ya watu kutoka nje viondolewe.
Waziri al Tamimi amesema kupitia taarifa kwamba maeneo kadhaa ya mji wa Baghadad yanayoaminika kuwa chanzo cha kusambaa kwa virusi yatafungwa kufikia Jumatano kwa kipindi cha wiki mbili.
Serikali mpya chini ya waziri mkuu Mustafa al-Kadhimi iliapishwa wiki mbili zilizopita kufuatia kuwepo ombwe la uongozi kwa kipindi cha miezi mitano.
Miongoni mwa ajenda kuu alizozipa kipaumbele waziri mkuu huyo ni jitihada za kukabiliana na mripuko huo wa virusi vya corona na mgogoro wa kiuchumi uliosababishwa na kuporomoka kwa bei ya mafuta.
Mpaka sasa kiasi watu 123 wamekufa miongoni mwa wagonjwa 3,404 waliothibitika kuambukizwa kirusi hicho.