Rais Vladimir Putin amezungumzia kuhusu athari za virusi vya corona katika sekta ya ajira nchini Urusi.
Kiongozi huyo amefanya mkutano na viongozi wa serikali kupitia video katika mji mkuu wa Moscow, akifanya tathmini juu ya soko la kazi nchini.
Akielezea kuwa soko la ajira ni moja wapo ya vipaumbele vyake, Putin amesema,
"Janga la Covid-19 limeathiri vibaya uchumi wa nchi zote duniani bila kuchagua.Mahitaji,biashara na uwekezaji vyote vimeporomoka."
"Takwimu za hivi karibuni zinaonesha kuwa idadi ya rasmi ya wasiokua na ajira nchini Urusi imeongezeka. Idadi ya wasio na ajira imeongezeka hadi milioni 1.9." alisema.
Uchumi wa Urusi, umekuwa ukikabiliwa na nyakati ngumu kwa sababu ya kushuka kwa bei ya mafuta pamoja na hatua zilizochukuliwa kupambana na maambukizi ya corona.
