Umoja wa Ulaya wasaka kuimarisha mkakati wake kuelekea China

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya wanatarajia kuimarisha mkakati wao kuelekea China hii leo, kukabiliana na diplomasia ya kimabavu ya China inayoongezeka na kuongeza juhudi za kuzuwia uingiaji wa kampuni za China barani Ulaya bila udhibiti wowote.

Katika wakati ambapo Beijing inakabiliwa na ukosoaji kuhusu namna inavyoshughulikia mzozo wa virusi vya corona, mawaziri hao wamejadiliana kwa mara ya kwanza kwa njia ya video kabla ya mikutano miwili ya kilele ya Umoja wa Ulaya na China ambayo inaweza kufanyika mwaka huu mmoja ukitarajiwa kufanyika mwishoni mwa Juni na mwengine Septemba.

Umoja wa Ulaya unajaribu kutafuta njia ya kati katika mzozo wa China na Marekani lakini ukiwa una mgawanyiko wa ndani kuhusu China huku baadhi ya mataifa yakiwa wananufaika wa ufadhili wake.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Ujuwe Ugonjwa wa Busha

Kilimo cha Bamia