Hong Kong yaadhimisha mwaka mmoja baada ya kuzuka maandamano

Hong Kong inafanya kumbukumbu leo ya mwaka mmoja tangu kuzuka kwa maandamano ya kudai demokrasia, kupigwa marufuku mikusanyiko wakati wa maambukizi ya virusi vya corona pamoja na ujio wa sheria ya usalama wa taifa inayozuwia machafuko yoyote kurejea katika mji huo.

Miezi saba ya maandamano makubwa yenye ghasia yalianza Juni 9 mwaka jana wakati zaidi ya watu milioni moja walipoingia mitaani kupinga mswada wa sheria inayoruhusu watu kupelekwa China bara wanapofanya makosa.

Makundi yanayosambaza ujumbe yanayotumiwa na waandamanaji yametoa wito kukusanyika hapa na pale jioni, licha ya kuwa maeneo ya kukusanyika yatatangazwa saa moja kabla ya wakati wa mkusanyiko huo.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items