Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binadamu Human Rights Watch limewataka wafadhili na washirika wa kigeni wa Sudan waishinikize nchi hiyo izingatie haki, sheria na mabadiliko kwenye taasisi, wakati serikali inapoendelea kutatua matatizo ya kiuchumi yanayoikabili nchi hiyo.
Mkutano ulioandaliwa na marafiki wa Sudan utafanyika leo Juni 25 mjini Berlin kwa ajili ya kuisaidia Sudan kiuchumi.
Mkurugenzi wa Afrika Mashariki wa shirika la Human Rights Watch Jehanne Henry amewataka viongozi wa Sudan pamoja na wa kimataifa kuutumia mkutano huo kupanga jinsi Sudan itakavyosonga mbele ili mabadiliko ya uongozi yaliyofanyika yaweze kufanikisha njia sahihi hasa kwenye masuala ya uongozi na haki za binadamu.
