Iran inapanga kuuza mafuta yake nje kupitia ghuba ya Oman

Iran inapanga kuuza nje mafuta yake kutokea katika bandari iliyoko katika pwani ya ghuba ya Oman ifikapo Machi mwakani, rais wa nchi hiyo amesema leo, ikiwa ni mabadiliko ambayo yataepusha kutumia ujia wa bahari wa Hormuz ambao umekuwa kitovu cha wasi wasi katika eneo hilo kwa miongo kadhaa.

Wasi wasi umeongezeka kati ya Tehran na Washington tangu mwaka 2018, wakati Marekani ilipojitoa kutoka makubaliano ya kinyuklia ya mwaka 2015 kati ya Iran na mataifa sita makubwa duniani na rais Donald Trump kurejesha vikwazo dhidi ya Iran, na kuathiri mauzo muhimu yake ya mafuta.

Iran mara kadhaa imetishia kufunga ujia huo wa bahari iwapo mauzo ya mafuta yake ghafi yatazuiwa na vikwazo vya Marekani, hatua ambayo Marekani imesema itafikia kuvuka msitari mwekundu na hatua hiyo itahitaji kupatiwa jibu.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia