Serikali ya Muafaka wa Kitaifa ya Libya yakataa pendekezo la usitishaji vita la Misri na Haftar



Jeshi la serikali ya muafaka wa kitaifa ya Libya limekataa pendekezo la kusitisha vita lililotolewa na Misri na vikosi vya mashariki mwa nchi hiyo na badala yake limesisitiza kudhibitiwakudhibitiwa maeneo yote ya nchi hiyo.

Muhammad Qanunu amesema kuwa serikali ya muafaka wa kitaifa ya Libya haina wakati wa kupoteza na kwamba  yenyewe itachukua uamuzi wa kusimamisha vita. Qanunu ameyasema hayo akijibu pendekezo la kusimamisha vita lililotolewa na Misri na Jenerali muasi Khalifa Haftar kamanda wa wanamgambo wa mashariki mwa Libya.

Msemaji wa jeshi la serikali ya muafaka wa kitaifa ya Libya ameongeza kuwa vikosi vya jeshi hilo vitaendelea kufanya kwa nguvu na irada kamili oparesheni ya kuwasaka wanamgambo magaidi wa Haftar. 

Rais Abdel Fattah al Sisi wa Misri na Jenerali Khalifa Haftar pamoja na Agula Saleh Spika wa bunge la mashariki mwa Libya lenye makao yake katika mji wa Tobruk jana baada ya kufanya mauzngumzo ya masaa kadhaa walitoa taarifa juu ya pande hizo kufikia muafaka kuhusu mpango wa kisiasa kwa ajili ya kusimamisha mapigano huko Libya. 


Vita vya niaba nchini Libya vimeshika kasi na ingawa vikosi vya Serikali ya Muafaka wa Kitaifa Libya vimepata ushindi mkubwa  na vinakaribia kupata ushindi wa mwisho na kuwadhoofisha kabisa wanamgambo na waasi, lakini hali ya kisiasa nchini Libya sambamba na kuwepo pande kadhaa za kitaifa na kimataifa ambazo zinataka kunyakua utajiri wa nchi hiyo ni kizingiti kikubwa katika kufikiwa utulivu na amani katika nchi hiyo. Kuhusiana na nukta hiyo, jamii ya kimataifa inaamini kuwa njia pekee ya kutatua mgogoro wa Libya ni kupitia mazungumzo baina ya makundi yote nchini humo.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia