Tetesi za soka leo Juni 2


Chelsea wanafikiria kubadili uamuzi wao kwa kumsaini mshambuliaji wa RB Leipzig Timo Werner,24, ikiwa Mjerumani huyo ataonesha nia utayari wa kuhama. (ESPN)

Mshindi mara sita wa tuzo ya Ballon d'Or Lionel Messi, 32, atasalia Barcelona msimu ujao baada ya kipengele cha mkataba wake kinachomruhusu mshambuliaji huyo wa Argentina kuondoka baada ya mkataba kuisha msimu huu (Standard)


Real Madrid wamekataa nafasi ya kumsajili winga wa Chelsea Willian, 31, kwa uhamisho huru.Mkataba wa mchezaji huyo wa Brazil unamalizika msimu huu. (Mirror)

Manchester United italipa pauni milioni 10.5 kwa ajili ya kuongeza mkataba wa kucheza kwa mkopo kwa mshambuliaji wa Nigeria Odion Ighalo mpaka mwezi Januari, ada ya pauni milioni 6 inakwenda Shanghai Shenhua na pauni 130,000 ni mshahara wa wiki. (Mail)

Liverpool wako kwenye majadiliano kuongeza mkataba wa kucheza kwa mkopo kwa kiungo wa Harry Wilson,23, wa Bournemouth na mshambuliaji wa kiingereza Rhian Brewster,20, wa Swansea mpaka mwishoni mwa msimu (Telegraph)


Arsenal wako tayari kumpatia mchezaji wa nafasi ya ulinzi David Luiz, 33, mkataba wa mwaka mmoja lakini watapunguza mshahara wake wa wiki (Mirror)

Kocha wa England Gareth Southgate hatahudhuria michezo ya ligi ya primia msimu utakapoanza kwa kuwa anahisi kuwa uwepo wake kwenye viwanja hauna umuhimu. (Star)

Chelsea imepeleka mapendekezo yake kwa ligi ya primia kuongeza idadi ya wachezaji wa kubadilisha wanaoruhusiwa kuwa kwenye benchi kuwa tisa badala ya saba katika kipindi hiki cha msimu uliobaki. (Mail)


Bayern Munich wanataka kumsajili winga wa Manchester City, raia wa Ujerumani Leroy Sane , 24,na Kai Havertz, 20, kutoka Bayer Leverkusen kama sehemu ya ''enzi mpya'' katika klabu, amesema Makamu Mwenyekiti. (Bayern1 via Evening Standard)

Chelsea inaiongoza Paris-St Germain katika kinyang'anyiro cha kumnasa beki wa kushoto wa Porto na raia wa Brazil Alex Telles, 27. (Tuttosport via Express)

Lille wamepata ofa nyingi kwa ajili ya mshambuliaji wao Osimhen. Tottenham, Liverpool na Arsenal ni miongoni mwa vilabu vinavyomtaka Mnaijeria huyo,21, (Mail)


Mshambuliaji wa RB Leipzig na mchezaji anayetolewa macho na Liverpool Tino Werner ameweka wazi uamuzi kuhusu mustakabali wake katika mazungumzo kuhusu uhamisho wake, ameeleza Mkurugenzi wa michezo wa Inter Milan Piero Ausilio. Ausilio amesema Mjerumani huyo, 24, ''hatakuja kwetu''. (Daily Star)

Arsenal wanapendelea kumpata mshambuliaji wa Napoli Arkadiusz Milik,26, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka Juventus (La Repubblica via Daily Star)


Kiungo wa Atletico Madrid na mchezaji anayefikiriwa pia na Manchester United Saul Niguez amesema atatangaza ''klabu mpya'' ndani ya siku tatu zijazo. Raia huyo wa Uhispania, 25, mkataba wake na timu ukitaka kuweka mezani kitita cha pauni milioni 130 ili kumnyakua .(Manchester Evening News)Kiungo wa kati wa Liverpool Harvey Elliot amekacha nafasi ya kujiunga na Real Madrid. Muingereza huyo, 17, alikuwa amealikwa kukutana na Sergio Ramos katika jaribio la kumshawishi kujiunga. (The Athletic)


Barcelona itatafuta pauni milioni 9 kama ada ya mkopo kutoka kwa klabu yoyote ya ligi ya primia kwa ajili ya kiungo wa kati na raia wa Brazil Philippe Coutinho.(Mundo Deportivo via Mirror)

Everton wanatarajiwa kumuita tena mlinda mlango Jonas Lossl, 31, baada ya mkataba wake wa kucheza kwa mkopo kumalizika katika klabu ya Huddersfield Town. (Yorkshire Evening Post)

Celtic wanafikiria kumsajili mlinda mlango wa Manchester City raia wa Chile Claudio Bravo, 37. (Times-in Spanish)

Kocha wa Chelsea Frank Lampard amesema ''atafanya maboresho '' katika kikosi chake katika dirisha kubwa la usajili (Mail)

Inter Milan wamesema kuwa wanataka kuendelea kumshikilia mshambuliaji wa Manchester United Alexis sanchez kwa mkopo baada ya tarehe 30 mwezi Juni. Mchezaji huyo anaichezea klabu hiyo ya ligi ya Serie A mpaka mwishoni mwa msimu. (Sky Sports Italia)