Idadi ya visa vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya corona Amerika ya Kusini imepindukia milioni moja, huku Uingereza na Urusi ambazo ziliathirika pakubwa na janga hilo zikiondoa taratibu vizuizi, licha ya kutodhibiti kikamilifu milipuko ya virusi hivyo.
Serikali kote ulimwenguni zimeanza kulegeza vikwazo ambavyo vimeathiri pakubwa uchumi wao, hata wakati idadi ya visa ikifikia milioni 6.1 na vifo vikipindukia 371,000.
Huku ikiwa na zaidi ya maambukizi nusu milioni, Brazil sasa ni nchi ya pili duniani kati ya zilizoathirika pakubwa na janga hilo, lakini rais wake anayepinga hatua za kusitishwa shughuli za maisha Jair Bolsonaro amekaidi mapendekezo ya kupiga marufuku mikusanyiko.
Nchini Uingereza, ambako baadhi ya shule zimeanza kufunguliwa tena hii leo, washauri kadhaa waandamizi wa serikali wanaonya kuwa mambo yanafanyika kwa kasi.
Urusi imeanza kufungua maduka na bustani za kustarehe mjini Moscow licha ya kuwepo bado visa vingi vya maambukizi. Nayo Uturuki imerusuhu tena kuanza safari za ndege za ndani ya nchi.