Waandamanaji wafanya maandamano makubwa ya amani ya kutaka mabadiliko



Maelfu ya waandamanaji walikusanyika katika mji mkuu wa Marekani Washington na miji mingine mikubwa nchini humo hapo jana, katika kampeini nyingine kubwa ya uhamasishaji dhidi ya ukatili wa polisi na ubaguzi wa rangi huku George Floyd akikumbukwa nyumbani kwao katika mji wa North Carolina.

Waandamanaji walifanya maandamano ya amani kote nchini humo na mabara mengine manne, yote kwa ujumla yakionesha kwa pamoja uhamasishaji mkubwa zaidi wa siku moja tangu mauaji ya Floyd siku 12 zilizopita mikononi mwa polisi katika jimbo la Minneapolis. Maandamano hayo makubwa, yalitamatisha wiki ya maandamano ya karibu kila siku katika kile ambacho taifa hilo halijashuhudia katika kizazi cha hivi karibuni.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia