Waziri mkuu wa Armenia agunduliwa kuwa na maambukizi ya Covid-19

Idadi ya watu ambao wamekwishafariki kutokana na maambukizi ya virusi vya corona ulimwenguni  imefikia watu  373 900 huku watu wengine zaidi ya milioni 6 wakiwa  na maambukizi ya virusi hivyo.

Watu ambao wamripotiwa tayari kupona maambukizi hayo tangu kaibuka kwa virusi hivyo idadi yake imefikia wa  2 848 000.

Nchini China , kitovu cha virusi hivyo  mwishoni mwa mwaka  2019,  watu  16 wamegunduliwa kuwa na maambukizi mapya  ya covid-19 ndani ya masaa  24.

Watu  4634 wamefariki nchini China kutokana na virusi hivyo .

Nchini Korea Kusini, watu  271 wamefariji  huku watu  35 wakiripotiwa kugunduliwa kuwa na maambukizi  na kupelekea idadi kuongezeka na  kutangazwa kuwa watu   11550.

Taarifa iliotolewa na eneo la wakurdi nchini Irak, taarifa hiyo imesema kwuwa  watu wawili wamefariki katika  mkoa wa Süleymaniye na Erbil.

Vipimo vilivyoendesshwa kwa watu  104 Süleymanye na Erbil , matokeo yake yameonesha kuwa  idadi ya kesi mpya za maamukizi inaongezeka.

Serikali imechukuwa hatua mpya ambazo malengo yake ni kukabiliana  na maambukizi  ya covid-19.

Agizo  na marufuku ya kutotoka nje imetangazwa upya  kwa kutolewa armi ya kufungwa maduku na vituo vyote vya biashara vilivyokuwa vimeruhusiwa kufungua na kuendelea na biashara.

Waziri  mkuu wa Armenia , Nikol Pashinyan  ametangaza kuwa  wanafamilia wake wote wamegunduliwa kuwa na maambukizi ya  virusi vya corona.

Kulingana na taarifa  zilizotolewa huenda waziri mkuu huyo aliambukizwa baada ya kushiriki katika mkutano wa kikazi.

Nchini India, watu  5408  wamefariki .

Nchini Pakistani watu   543 wamefariki kutokana na maambukizi ya virusi hivyo .
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia