WHO limesema linapata uungwaji mkono inaouhitaji

Ufaransa na Ujerumani zimeeleza uungaji wao mkono mapambano ya shirika la afya ulimwenguni WHO dhidi ya virusi vya corona leo, ambapo Ujerumani imesema itachangia kiasi ya euro nusu bilioni katika bajeti ya shirika hilo la Umoja wa mataifa.

Mkuu wa shirika la WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus, akizungumza katika mkutano na waandishi habari, amesema shirika hilo, lililokosolewa kwa kiasi kikubwa na Marekani, linapata msaada wote wa kifedha na kisiasa linaouhitaji.

Zaidi ya watu milioni 9.44 wameripotiwa kuwa wameambukizwa virusi vya corona duniani na watu 481,672 wamefariki, kwa mujibu wa idadi iliyowekwa pamoja na shirika la habari la Reuters.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia