Njia sahihi ya kuikuza biashara yako

Kwa Kuwa kuna usemi  wanasema wengi wape na kwaku kuwa takwimu sinatuambia  idadi kubwa ya watu ni wafanyabiashara ni vyema tukakumbiashara baadhi ya mambo ya msingi yatakayotufanya ili kukuaza biashara zetu . Na asilimia 40 ya watu ambayo hawafanyi  biashara ni muda wao na wenyewe kujifunza ili waweze nao kuwa wafanyabiashara wazuri.

Moja ya changamoto kubwa inayokuwakumba wafanyabiashara walio wengi ni kutokujua kiundani juu ya biashara yake hata hivyo idadi kubwa ya wafanyabiashara hao biashara zao huwa haziwi za muda mrefu na hata pale zinapokuwa za muda mrefu huwa hazikui. Nakusihi ufuatane nami mwanzo hadi mwisho ili kuweza kuona biashara yako inakuwa na Maisha marefu na yenye kukua.

1.  Ongeza maarifa kwa kujifunza.
Kama kweli unahitaji Mafanikio zaidi ya kiabiashara ni vyema ukawa ni mtu wa kujifunza kuhusiana na biashara yako. Ni lazima ujifunze mbinu mbalimbali ambazo wanazitumia wafanyabiashara wengine. Kujifunza huku kujupe muda muafaka wakugundua pale ambapo wafanyabiashara engine wanafeli. Baada ya kujua wanafeli wapi kwako ifanye kama fursa kama fursa ya kuboresha biashara yako. Kufanya hivo kutakufanya uongeze wateja kwani utakuwa mbunifu zaidi.

2. Badili tabia zako.
Moja ya chachu nzuri ya kukufanya ukuwe kibiashara ni lazima uweze kujua vizuri tabia yako. Inawezekana wewe unajiona upo sawa ila kumbe sivyo unavyofikiri. Hata hivyo ili kuweza kujua ni ipi tabia yako ni vyema ukafanya uchunguzi ili kujua watu wanakuzungumziaje wewe? Kufanya hivo kutasaidia kwa sababu watu wengine ndio wana picha kamili juu ya wewe ni biashara kwa ujumla. Pia ili kuweza kufanikiwa ni lazima uweze kubadili tabia uliyonayo ya uvivu na ongeze juhudi za kiutendaji katika kufanya kazi.

3. Tenga muda wa kufukiri kuhusu biahara yako.
Moja ya mbinu ya kuweza kukuza biashara yako ni kuweka muda kwa ajiri ya kujua biashara yako inakwenda vipi. Biashara zilizo nyingi huwa hazina Maisha marefu kwa sababu wahusika hawan muda wa kutosha kuhusu kufikiri njinsi gani biashara inakwenda bali walio wengi hutazama faida tu. Kufanya hivyo tambua biashara yako hatakuwa na Maisha marefu ni vema ukawa mzuri kujua utendaji wako wa kibiashara na changamoto zake na jinsi ya kutatua.

4. Tambua mchango wako wa watu wengine.
Ukitaka kufanikiwa zaidi ni vema ukajua ni kwa jinsi unavyojenga mahusiano na wafanyabiashara  na wateja pia. Mchango mzuri uliona nao utakufanya uongeze wateja wengine. Kwa mfano unauza biashara fulani ghafla ukaishwa bidhaa fulani harafu mteja akaja kuuliza bidhaa hiyo, usimwambia mteja huyo kwamba kama huna bidhaa hiyo mwambie ngoja nikakuchukulie kwenye stoo. Na kwa kuwa wewe huna bidhaa hiyo nenda kwa jirani yako nenda ukanunue na uje kumpa mteja huyo. Kufanya hiyo kutakufanya uweze kujenga mahusino na wafanyabiashara nyingine pia njia ya kuongeza wateja na kufanikiwa zaidi.

5. Usiridhike na hali uliyonayo.
Kuwa mfanyabiashara mkubwà ni lazima kuwa katika imani ambyo hakulishi. Maana yangu hata kama wewe unajiona tayari umefanikiwa wewe jione bado una kiu ya kufanikiwa zaidi. Kama wasemavyo kwamba pesa haitoshi basi hata wewe una deni la kufanikiwa zaidi. Moja ya kufeli kwa biashara ni pale mtu anapoona amepata Mafanikio na yeye anaridhika . kuridika ni adui wa Mafanikio. Kuridhika ndiko kunako turudisha nyuma watu wengi sana. Pia nikumbushe ya kwamba kufeli sio kushindwa ni sehemu ya mafanikio.

Endelea kutembelea Muungwana Blog kila wakati.

Na. Benson Chonya.