Serikali imeeleza kuwa familia ya Marehemu Mzee Majuto na Steven Kanumba zimelipwa fedha zinazo tokana na kazi zao walizoziacha ambapo serikali imechukua jukumu la kufuatilia mikataba ya kazi zao.
Hayo yamesema leo na katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi akiongoza hafla ya uhamishaji wa COSOTA kutoka Wizara ya Viwanda kwenda Wizara ya Habari ili kuziweka pamoja mamlaka zinazosimamia wasanii.
“Familia ya Marehemu Mzee Majuto mpaka sasa tumewarejeshea TZS milioni 65 na familia ya Marehemu Steven Kanumba tumeirejeshea TZS milioni 20 kutoka katika mikataba ya kazi waliyokuwa wameingia.” amesema Dkt. Hassan Abbas.
Katika hatua nyingine Dkt. Abbas amesema, “Tumshukuru Rais John Magufuli kwa sababu huu mjadala wa kwanini COSOTA ipo Wizara ya Viwanda umekuwa mrefu tangu nikiwa chuo. Lakini ndani ya saa 24 tangu Julai 12, 2020, Rais alisaini hati ya kuihamishia COSOTA Wizara ya Habari.”
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Prof. Riziki Shemdoe amesema, “Tumehamisha taasisi hii (COSOTA) kwenda Wizara ya Habari lakini nisisitize kuwa tutaendelea kushirikiana maana ni serikali moja. Na mtakapo kwenda Wizara ya Habari mkaendeleze yale yote mazuri mliyokuwa mnayafanya.”